Shuhuda & Mrejesho

Shuhuda

Habari za Maendeleo

Vizimba vya kubulia samaki Mwanza

Francis Kajubi

Francis Kajubi

Mshindi Sekta ya Fedha na Uchumi 2025

Mashindano haya ya SKA ni muhimu yakiendelezwa hata kushirikisha taasisi za kimataifa, kwa kutoa sapoti kwa sababu mashindano haya yanaleta chachu ya uandishi wa habari za kizalendo. Habari nyingi zipo nzuri zinazohusu mambo ambayo serikali inafanya lakini waandishi inakuwa ngumu kuzifikia kwa sababu zipo mbali vijijini na waandishi wanakuwa hawana uwezo wa kuzifikia kule, kwa hiyo watokea wadau wakisapoti habari hizi zitaandikwa kwa wingi sana. Kumekuwa na mwitikio mkubwa wa kuandika habari za kizalendo tangu Tuzo hizi zilipotolewa mimi nikifuatilia kwenye vyombo vya habari naona waandishi wamekuwa wakiandika zaidi habari za ndani

Mathias Kanal

Mathias Kanal

Mshindi Sekta ya Ujenzi 2025

Napendekeza katika kuboresha uandishi wa habari za maendeleo ni muhimu kuwe na mafunzo ya mara kwa mara kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa, ili kuwajengea uwezo waandishi kuongeza ubora wa kazi zao za uandishi

Joshua Sengo

Joshua Sengo

Mshindi Afisa Mabari Mahiri wa Serikali 2025

“Niwaombe waandishi wenzangu pamoja na maafisa Habari wa taasisi za Serikali na binafsi kutekeleza wajibu wetu kwa bidii, kuhabarisha wananchi kuhusu fedha zinazotolewa na serikali na namna zinavyotumika katika maendeleo ya jamii. Serikali imetoa fedha nyingi kwenye Halmashauri kwa ajili ya Afya, Maendeleo ya Jamii, miundombinu, elimu msingi na sekondari na sekta nyingine lakini wananchi bado hawajui kama kuna fedha ambazo zinapelekwa kwa ajili ya miradi ya Maendeleo.”

Mrejesho

Maoni Yako Yana Thamani!!

Tunakaribisha maoni, mapendekezo, na uzoefu wako ili kuboresha Tuzo za Samia Kalamu Awards kwa mwaka ujao.

3+

Maoni Yaliyopokelewa