Habari

Rudi kwenye habari
SAMIA KALAMU AWARDS 2026 KUTOLEWA DESEMBA

SAMIA KALAMU AWARDS 2026 KUTOLEWA DESEMBA

18 Novemba 2026

Waandishi wa Habari 64 na Vyombo vya Habari 11 Wafuzu Kuwania Tuzo za Samia Kalamu 2026

Dar es Salaam, 17 Novemba 2026

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), tunawataarifu waandishi wa habari na umma kwa ujumla kwamba mchakato wa kuwapata washindani waliofuzu kuingia hatua ya mwisho ya Tuzo za Uandishi wa Habari za Maendeleo (Samia Kalamu Awards 2026) umekamilika.

Jumla ya waandishi wa habari sitini na nne (64) wamefuzu kuingia hatua hiyo, pamoja na vyombo vya habari kumi na moja (11).

Tuzo hizi zinajumuisha Tuzo za Kisekta, Tuzo kwa Vyombo vya Habari na Tuzo Maalumu za Kitaifa. Washindani waliofuzu wamepatikana kupitia mchakato wa upigaji kura wa umma na tathmini ya majaji kumi na tisa (19) waliobobea katika taaluma za uandishi wa habari, mawasiliano kwa umma na uhusiano wa umma.

Hafla ya kuwatunuku washindi inatarajiwa kufanyika tarehe 5 Desemba 2026, katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

USHIRIKI NA TATHMINI YA KAZI

Jumla ya kazi elfu tatu na tatu (3,003) ziliwasilishwa kuwania Samia Kalamu Awards 2026. Baada ya tathmini ya majaji, kazi mia nane themanini na mbili (882) zilifuzu kuingia katika hatua ya upigaji kura wa umma. Katika hatua hiyo, jumla ya kura laki tatu kumi na saba elfu mia tatu tisini na tisa (317,399) zilipigwa, zikionesha mwitikio mkubwa wa wananchi katika kutambua na kuthamini uandishi wa habari za maendeleo.Tuzo hizi zinatoa fursa kwa waandishi wa habari, maafisa habari na vyombo vya habari kushindana na kutambuliwa kwa ubora wa kazi zao zilizochapishwa au kurushwa hewani ndani ya kipindi kilichoainishwa katika mwongozo wa tuzo. Ushiriki wao, pamoja na mwitikio wa wananchi, unaonesha umuhimu wa tuzo hizi katika kuhamasisha uandishi wa habari unaochangia maendeleo ya jamii na taifa.

Tathmini ya majaji ilizingatia vigezo vilivyobainishwa katika mwongozo wa tuzo, vikiwemo ubora wa maudhui, uzingatiaji wa maadili ya taaluma, matumizi ya utafiti na takwimu, athari chanya kwa jamii na mchango katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (Dira 2050).

UJUMBE KWA WASHIRIKI NA WAGENI WAALIKWA

Orodha ya waandishi wa habari na vyombo vya habari waliofuzu kuingia katika hatua ya mwisho ya Samia Kalamu Awards 2026 imeambatishwa katika taarifa hii na inapatikana pia katika tovuti ya tuzo, www.samiaawards.tz. Washiriki waliofuzu watapokea maelekezo kuhusu ushiriki wao katika hafla hiyo kutoka kwa Kamati ya Maandalizi ya tuzo.

KUHUSU SAMIA KALAMU AWARDS

Samia Kalamu Awards (SKA) ni jukwaa maalumu la kitaifa lililoasisiwa mwaka 2024 kwa lengo la kutambua, kuenzi na kuhamasisha ubora, weledi na ubunifu katika uandishi wa habari na makala za maendeleo nchini. Tuzo hizi zinaratibiwa na TCRA kwa ushirikiano na TAMWA na JAB kama sehemu ya juhudi za kukuza uandishi wa habari unaochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kupitia kaulimbiu ya tuzo kwa mwaka 2026 “Kalamu kwa Maendeleo”, SKA inahimiza uzalishaji wa maudhui ya ndani yenye ubora, yanayozingatia utafiti na takwimu, usahihi, weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari. Aidha, tuzo hizi zinatambua mchango wa waandishi wa habari na vyombo vya habari katika kuhabarisha na kuelimisha umma kuhusu maendeleo ya taifa, kuhamasisha uwajibikaji na kuimarisha taswira chanya ya Tanzania ndani na nje ya nchi.

Hafla ya kwanza ya utoaji wa tuzo hizi ilifanyika mwaka 2025 na mwaka 2026 ni msimu wa pili.

Kwa maelezo zaidi, tembelea www.samiaawards.tz au wasiliana na Kamati ya Maandalizi kupitia ska@tcra.go.tz.

 IMETOLEWA NA:

Kamati ya Maandalizi ya Samia Kalamu Awards 2026
TCRA | TAMWA | JAB

KIAMBATISHO NA 1: Waandishi wa Habari Waliofuzu Kuwania SKA-2026

  1. Adela Madyane -TBC

  2. Rajabu Mustafa Mrope - Pangani FM

  3. Jamaldini Abuu Zuberi - TBC

  4. Jesse Mbezi Mikofu- Mwananchi

  5. Nusra Shaaban Juma - Zanzibar Leo

  6. Sanula Renatus Athanas- Nipashe

  7. Christine Stephen Mwakangale - The Guardian Ltd

  8. Julius M Maricha- The Citizen

  9. Rahma Suleiman Ali - Nipashe

  10. Mnaku Bernard Mbani - The Guardian Ltd

  11. Joseph Ernest Nakajumo - Uhuru Publications Ltd

  12. James Albert Kandoya - The Guardian Ltd

  13. Halfan Ramadhani Chusi- Nipashe

  14. Riziki Abdalla Ali- Zanzibar Leo

  15. Esco Donald Mkandawile- Simulizi na Sauti

  16. Emmanuel Bwighane Kalemba- Azam Media

  17.  Elesia Thomas Haule- Azam Media

  18. Maregesi Evarist Paul - Pambazuko Newspaper

  19. Aveline Kitomary- TSN

  20. Rosemary Joseph Mirondo- The Citizen

  21. Yusuph Michael Mazimu- BBC

  22. Mussa Yusuph Mussa- Uhuru

  23. Isack Dickson Lukumay-Orkonerei FM

  24. Gervas Charles Mwatebela - TBC

  25. Saada Amir Mlagwa - Mwananchi

  26. Beatrice Moses Kabojoka - The Guardian

  27. Rahel Japhet Pallangyo- Habari Leo

  28. Mathias Said- Wazohuru Media

  29. Khamisuu Abdallah Ali - Zanzibar Leo

  30. Baraka Loshilaa- Mwananchi

  31. Asya Hassan Bakar- Zanzibar Leo

  32. Gwamaka Mwaipungu Alipipi- Nipashe

  33. Emmanuel Omondi Onyango- The Guardian

  34. Ramadhani Ismail Nyassa- The Citizen

  35. Josephine Sebastian - The Citizen

  36. Esther Assimwe- TBC

  37. Beatrice Philemon Mukocho -The Guardian

  38. Vuai Makame - Tumbatu FM

  39. Neema Emmanuel Abel-Nipashe

  40. Gadiosa Lamtey- The Citizen

  41. Aurea Simtowe- Mwananchi

  42. Sameer Ahmed -TBC

  43. Ngarayai Ole-Kimosa -TBC

  44. Innocent Anselemi -Tumaini Media

  45. Simon Mkina -Pambazuko

  46. Fatma Chikawe -Azam Media

  47. Eliya Marohe -Mwananchi

  48. Ally Mbogo Mayala - TSN

  49. Maureen Minanago- TBC

  50. Ahmada Juma- The Daily News

  51. Daniel Samson- Nukta Africa

  52. Rose Yolam Masaka- TBC

  53. David Katimbila Geke-TBC

  54. Shaban Hamisi Njia- Nipashe

  55. Tuma Dandi- TBC

  56. Albano Maganga Midelo- Habari Leo

  57. Harith Ally- Watetezi TV

  58. Esau Ng'umbi- Nukta Africa

  59. Marco Zephania Maduhu - Nipashe

  60. Bakari Chijumba - Ayo TV

  61. Ichikael Leonard Malisa - Afisa Habari - Njombe

  62. Adam Gabriel Hhando - Afisa Habari -Tanga

  63. Albano Maganga Midelo- Afisa Habari -Ruvuma

  64. Francis Kajubi -The Guardian Ltd

 

  Kiambatisho Na 2: Vyombo vya Habari Vilivyofuzu Kuwania SKA-2026  

 

  1. Azam 4 HD

  1. Safari Channel

  2. Orkonerei FM

  3. Mpanda FM

  4. Mlimani FM

  5. Mwananchi

  6. Nipashe

  7. Uhuru

  8. Habari Leo

  9. The Citizen

  10. Mlimani TV

 

 

 

 

 

 

 

 

Picha (1)

5 Desemba 2026

Hafla ya Utoaji Tuzo za Samia Kalamu 2026

Mgeni Rasmi: Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

--Siku
--Saa
--Dakika
--Sekunde